Tabianchi na mazingira

Utunzaji wa viumbe anuwai unahimizwa na UM kwa natija za wote kimataifa

KM Ban Ki-moon na Raisi wa Baraza Kuu Srgjan Kerim wametoa onyo la pamoja wiki hii lenye kutahadharisha kwamba bila ya walimwengu kutunza mazingira ya viumbe na uhai anuwai, matokeo yake yatasababisha athari mbaya kimaisha, hali ambayo itaharibu na kuchafua pakubwa shughuli za uchumi, huduma za maendeleo na zile juhudi za kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa, takriban kote ulimwenguni. Onyo hili liliwasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira, Achim Steiner, kwa niaba ya KM na Raisi wa Baraza Kuu kwenye mkutano wa kusailia sera za kutunza kipamoja viumbe anuwai, unaofanyika mjini Bonn, Ujerumani.

UNEP imependekeza miti bilioni 7 ioteshwe duniani kuhifadhi mazingira

Achim Steiner, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) alipokutana na waandishi habari wa kimataifa hapa Makao Makuu Ijumanne, alitangaza kuanzishwa kampeni mpya iliokusudiwa kuuhamasisha umma wa kimataifa kupandisha miti bilioni 7 katika miezi 18 ijayo.

Dokezo ya kikao cha kuzingatia haki za wenyeji wa asili

Kuanzia tarehe 21 Aprili wajumbe 3,000 ziada waliowakilisha zile jamii zijulikanazo kama wenyeji wa asili, kutoka katika kila pembe ya dunia, walikusanyika hapa Makao Makuu kuhudhuria kikao cha mwaka, cha saba ambacho KM wa UM Ban Ki-moon alikiita \'kikao cha kihistoria kilichofikia njia panda\'. Majadiliano ya mkutano wa wenyeji wa asili yalichukua wiki mbili, na yanatazamiwa kukamilishwa Ijumaa ya leo.