Tabianchi na mazingira

Hapa na Pale

Mkutano wa Saba wa Tume ya Kudumu ya Wenyeji wa Asili umeingia kwenye wiki ya pili ya majadailiano katika Makao Makuu, ambapo masuala yanayotiliwa mkazo zaidi ni yale yanayoambatana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa umma wa kimataifa.

Tume ya Kudumu ya Wenyeji wa Asili yakutana Makao Makuu katika kikao cha mwaka

Kikao cha Saba cha Tume ya Kudumu ya UM juu ya Masuala ya Haki za Wenyeji wa Asili, kitakachochoendelea kwa wiki mbili, kilifunguliwa rasmi Ijumatatu, Aprili 21 kwenye Makao Makuu mjini New York. Mada ambayo inatarajiwa kupewa umuhimu zaidi mwaka huu ni ile inayoambatana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwenye tamaduni maumbile na namna inavyodhuru uwezo wa wananchi wa asili kujipatia riziki za kuendesha maisha.

FAO imehadharisha, upungufu wa chakula ukiselelea duniani machafuko yatashtadi

Jacques Diouf, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Chakula,na Kilimo (FAO) alitoa onyo maalumu hapo Ijumatano wakati alipokuwa anazuru Bara Hindi, ambapo alitahadharisha ya kuwa ulimwengu unawajibika kudhibiti kidharura hatari ya mifumko ya machafuko na vurugu, ambayo huenda ikachochewa na cheche mchanganyiko zinazotokana na kupanda kwa bei ya nishati kwenye soko la kimataifa, pamoja na ongezeko la mahitaji ya chakula duniani, na pia kuenea kwa tibuko la hali ya hewa ya kigeugeu katika ulimwengu, ikijumuika na matumizi ya kihorera ya ardhi ya kulimia kuzalisha nishati ya viumbe hai.

WMO yasisitiza 'Afrika itahitajia vifaa vya kisasa kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa'

Michel Jarraud, KM wa Shirika la UM juu ya Upimaji wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) aliwaambia wajumbe waliohudhuria kikao kinachozingatia masuala ya fedha na uchumi katika Afrika, kinachofanyika sasa hivi Addis Ababa, Ethiopia, kwamba bara la Afrika linahitajia kufadhiliwa kidharura uwezo na vifaa vya kisasa ili kudhibiti bora mabadiliko ya hali ya hewa.