Tabianchi na mazingira

Mkutano wa Bangkok unajadilia udhibiti mpya wa mabadiliko ya hali ya hewa

Ijumatatu, wajumbe wanaokadiriwa 1,200 kutoka Mataifa Wanachama 160 ziada walijumuika mjini Bangkok, Thailand kuanza duru ya kwanza ya mazungumzo ya siku tano, yanayoungwa mkono na UM, kuzingatia na kusailia mapatano mapya ya kudhibiti bora athari za mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Karibu watu milioni wamedhurika mwaka huu na mafuriko, vimbunga kusini mwa Afrika - UM

Ripoti mpya ya Ofisi ya UM inayohusika na Misaada ya Dharura Dunaini (OCHA) imeeleza ya kuwa watu karibu milioni moja wanaoishi katika mataifa ya Kusini mwa Afrika walisumbuliwa na kudhurika kihali mwaka huu kwa sababu ya mvua kali zisio za kawaida ambazo zilisababisha mafuriko na vimbunga haribifu.

UM unaadhimisha Siku ya Maji Safi/Salama Duniani

Ijumamosi tarehe 22 Machi huadhimishwa kila mwaka na UM kama ni Siku ya Maji Safi na Salama Duniani, na mada ya mwaka huu inatilia mkazo huduma za usafi. Taadhima hizi ni miongoni mwa juhudi za kuamsha hisia za umma wa kimataifa kwa kukumbushana ya kuwa watu bilioni 2.6 ulimwenguni bado hawakujaaliwa uwezo wa kupatiwa usafi wa kudhibiti afya. Mwaka huu UM umeyahimiza mataifa kuongeza zile huduma za kudhibiti bora matatizo yanayosababishwa na uchafu wa makaro yenye kuharibu vyanzo vya maji safi.

Mitambo ya simu kutoka ITU inahudumia waathiriwa wa mafuriko Zambia

Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Mawasiliano ya Kimataifa (ITU) limepeleka Zambia mitambo 25 inayobebeka ya satalaiti, kwa ajili ya kutumiwa kufufua tena shughuli za viunganishi vya mawasiliano ya simu, huduma ambazo ziliharibiwa sana na mafuriko makali yaliopiga karibuni taifa hilo.

UNEP inakhofu majabali ya barafu duniani yanayeyuka kwa kasi

Taasisi ya Utafiti wa Hali ya Majabali ya Mabarafu Duniani iliopo kwenye Chuo Kikuu cha Zurich, Uswiss na na ambayo huungwa mkono na Shirika la UM juu ya Hifadhi ya Mazingira (UNEP) imeripoti kuwa baina ya miaka ya 2004 hadi 2006, majabali haya ya barafu yameonekana kuyayuka kwa kasi iliozidi mara mbili kiwango cha wastani, kutokana na athari haribifu za mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Majabali haya ya barafu ni chanzo muhimu cha maji kwa mabilioni ya umma wa kimataifa.

UNICEF yahudumia kidharura waathiriwa wa Tufani Ivan Bukini

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF) limo mbioni kuifadhilia Bukini huduma za kihali, baada ya Tufani Ivan Maututi kupiga kwenye eneo hilo mwezi uliopita, na kuangamiza makazi ya watu karibu 200,000. Hivi sasa UNICEF inafadhilia makumi elfu ya waathiriwa madawa, vyandarua, mablangeti pamoja na vifaa vya huduma ya afya.