Habari Mpya

Niger ni mamuma:Benki ya Dunia

Ikiwa leo ni siku ya mtoto wa Afrika, ndoto za kutimiza ajenda ya bara hilo ya mwaka 2040 ya kuwa na bara la Afrika linalomfaa mtoto wa Afrika ikiwemo katika suala la kupata elimu, kwa Niger huenda lisitimie kwani asilimia 99 ya watoto wenye umri wa miaka 10 ni wajinga wa kutokujua kusoma na kuandika kulikoni.

 

Teknolojia imetuokoa wakati wa COVID-19 kusaidia jamaa nyumbani:DKT.Minja

“Zile fedha ambazo tunazituma zinamchango mkubwa sana sio tu kwa familia hata kwa jamii nzima kwa ujumla kwa maana ya kiuchumi , tunajua kwamba mathalani nchi ya Tanzania ilipokea dola Zaidi ya milioni 400 mwaka jana na nchi Jirani ya Kenya ilipokea dola za Kimarekani Zaidi ya bilioni 3 mwaka jana 2020.”  Dkt. Frank Minja 

Utumaji fedha kimtandao ulinusuru familia za kijijini mwaka 2020 

Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD umesema ingawa kiwango cha wahamiaji kutuma fedha nyumbani kimtandao  wakati wa janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 mwaka 2020 kimeongezeka, bado kaya za vijijini zilishindwa kunufaika vyema na utumaji huo kutokana na kukosa miundombinu ya kidijitali ya kupokea fedha hizo. IFAD imesema hayo ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya familia kutumiana fedha.

Dola Milioni 135 zatolewa na UN kusaidia wanaokabiliwa na Njaa

Umoja wa Mataifa umetoa dola milioni 135 kutoka kwenye Mfuko wake wa dharura (CERF) ili kuongezea kwenye shughuli za kibinaadamu katika nchi 12 barani Afrika, Amerika na Mashariki ya Kati, amesema Mratibu wa Mfuko huo Bwana Mark Lowcock akiwa mjini New York, Marekani.

 

Janga la COVID-19 limeongeza ukatili dhidi ya wazee: mtaalam wa UN aonya

Wakati mitazamo ya zamani kuhusu uzee tayari inadhoofisha uhuru wa wazee katika kufanya uchaguzi na maamuzi yao wenyewe, janga la COVID-19 limeleta zahma zaidi, dhuluma na kutelekezwa dhidi watu hao, ameonya leo mtaalam huru wa  haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, katika ujumbe wake kuhusu Ulimwengu siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhudu ukatili dhidi ya wazee.

Hatutoi Taarifa za wakimbizi kwa serikali ya Bangladesh bila ridhaa ya Wakimbizi wenyewe : UNHCR

Shirika la umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR kupitia tarifa yake kwa vyombo vya habari hii leo mjini Geneva Uswisi limesema halikusanyi taarifa za wakimbizi wa Rohingya waliopo Bangladesh na kuipa serikali bila idhini ya wakimbizi wenyewe na iwapo wakimbizi hao watakataa kutoa ruhusa basi watapatiwa mahitaji muhimu kama wale waliokubali bila kubaguliwa kwa aina yeyote. 


 

Wafanyakazi wa ndani bado wanalilia maslahi yao: ILO

Licha ya muongo mmoja wa uwepo wa mkataba wa kimataifa wa haki za wafanyakazi wa ndani,  bado kada hiyo inaendelea kupigania usawa na mazingira bora ya kazi huku janga la ugonjwa wa Corona au COVID19 likionesha dhahiri udhaifu uliopo katika kada hiyo.

Maelfu ya waliotawanywa na volkano DRC wahitaji msaada wa haraka:UNHCR

Mamia kwa maelfu ya watu waliotawanywa na mlipuko wa volcano wa mlima Nyiragongo Masharki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, sasa wanahitaji msaada wa haraka katika maeneo walikokimbilia na kupata hifadhi kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Flora Nducha anasimulia zaidi 

UN na zoezi la kijeshi kuimarisha vikosi vya Lebanon, kulikoni?

Huko nchini Lebanon, ujumbe wa kikosi cha mpito cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, umefanya mazoezi ya siku tano pamoja na vikosi vya usalama vya taifa hilo, LAF kama sehemu ya kujengea uwezo jeshi hilo la kitaifa kwa ajli ya kuimarisha amani na usalama.
 

UN imelaani vikali shambulio la kutisha hospitali nchini Syria

 Maafisa wakuu wa Umoja wa Mataifa leo wamelaani vikali shambulio baya lililofanyika katika hospitali nchini Syria mwishoni mwa wiki na kusisitiza haja ya uwajibikaji kwa uhalifu uliofanywa katika vita vya miaka kumi vya nchi hiyo.