Mashariki ya Kati

Rais wa Baraza Kuu kulaani kufunguliwa mashtaka Bashir

Rais wa Baraza Kuu la UM Balozi Miguel d\'Escoto Brockman, akizungumza na waandishi habari mjini Geneva amesema UM haujatengwa kutokana na kundi la mataifa tajiri na yanayoinukia G20 yanakutana kando.

UM wahimiza watu kuunga mkono kukomesha biashara haramu ya kuwauza binadamu

UM umezindua kampeni mpya, inayowakilishwa na utepe wa bulu ulochorwa kama moyo katika lengo la kuwahamasisha watu juu ya mamilioni ya waathiriwa wa biashara haramu ya kusafirisha binadamu, na kuwapatia uungaji mkono kupambana na tabia hii ambayo na utumwa wa mambo leo.

Lazima kukomesha ghasia dhidi ya wanawake asema KM

KM Ban Ki-moon amerudia tena mwito wake wa dharura wa kukomesha ghasia dhidi ya wanawake akieleza ni adhabu ambayo athari zake ni uchungu usoweza kupimwa.

Libya itazingatia sera ya kulinda amani na Sudan wakati inaongoza Baraza la Usalama

Libya inasema miongoni mwa masuala itazingatia mnamo mwezi huo inaposhikilia uwenyekiti wa Baraza la Usalama la UM ni sera ya kazi za kulinda amani na athari zinazoweza kutokea, kutokana na uwamuzi wa Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa kutoa kibali cha kukamatwa kwa Rais wa Sudan.

Baada ya mkutano wa wafadhili juu ya Ghaza msaada bado unazuiliwa

UM unaripoti kwamba licha ya mwito katika mkutano wa wafadhili wa kuruhusu bila kipingamizi chechote msaada kutoka njee pamoja na vifaa vya ujenzi kuingia katika kanda ya Gaza iliyoharibiwa kwa vita, maafisa wa uslama wa Israel wanaendelea kuzuia bidhaa muhimu kuingia.

UM unaeleza kua mzozo wa kifedha utazidisha umaskini

Utafiti mpya wa Umoja Ma mataifa unaeleza kwamba mzozo wa kifedha duniani unaokumba masoko ya fedha ya Marekani na Ulaya utawathiri watu fukara duniani na kuwatumbukiza mamilioni katika umaskini zaidi na kupelekea vifo vya maelfu ya watoto.

Mabadiliko ya hali ya hewa kuweza kuathiri sana uvuvi duniani

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo limechapisha ripoti hii leo ikionya kwamba ni lazima biashara ya uvuvi na idara za kitaifa za uvuvi zichukuwe hatua zaidi kufahamu na kujitayarisha kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa uvuvi duniani.

Simu za mkono njia muhimu ya mawasiliano kwa mataifa maskini

Sita kati ya kila watu kumi kote duniani wanasimu ya mkono ikiwa ni ishara kwamba simu hizo ndizo teknolojia ya mawasiliano iliyochaguliwa hasa katika mataifa maskini, hiyo ni kufuatana na ripoti mpya ya UM.

Kikao cha 10 cha Baraza la Haki za Binadamu cha funguliwa Geneva

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Navi Pillay, ameyahimiza tena mataifa ya dunia kuweka kando tofuati zao na kufanya kazi pamoja kuhakikisha matokeo ya ufanisi katika mkutano wa mwezi ujao dhidi ya kutostahamiliana, ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni huko Geneva.

KM anasema, amani ya kudumu ni lazima iwe msingi wa kuikarabati Ghaza

KM wa UM Ban Ki-moon ametoa mwito kwa wafadhili wa kimataifa kutoa fedha zinazohitajika sana kwa ajili ya kazi za kuikarabati Ghaza kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel. Bw Ban alisisitiza kwa mara nyingine tena haja ya kupatikana makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano na makubaliano jumla ya amani.