Habari Mpya

UNHCR kuhudumia maelfu ya wahamiaji wa Usomali walioathiriwa na mafuriko nchini Kenya

Shirika la UM juu ya Wahamiaji (UNHCR) limeripotiwa kushiriki hivi sasa kwenye shughuli kuhudumia misaada ya kihali kwa maelfu ya Wasomali walioathirika na maafa ya mvua kali zilizojiri karibuni katika eneo la kaskazini-mashariki ya Kenya, hususan katika zile kambi za wahamiaji za jimbo la Dadaab. Kwa mujibu wa UNHCR mvua hizo zilizusha mafuriko yalioeneza uharibifu mkubwa katika sehemu hiyo ya nchi.~

KM ahimiza kuwepo ushikiriano wa kimataifa kuisaidia Afrika kuepukana na umasikini

KM Kofi Annan Alkhamisi alitoa risala maalumu mjini Addis Ababa, Ethiopia mbele ya wajumbe waliohudhuria Mkutano juu ya Maendeleo ya Afrika, ambapo alionya ya kwamba pindi wahisani wa kimataifa watashindwa kushirikiana na UM pamoja na mataifa yanayoendelea kuisaidia Afrika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kuna hatari ya bara hilo kunyimwa huduma za kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii na, hatimaye, hata kunyimwa fursa ya kuyafikia, kwa wakati, yale Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs).

Baraza Jipya la Haki za Kiutu laelekea wapi kikazi?

Hivi karibuni Baraza la Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Kiutu, lenye wajumbe wanachama kutoka Mataifa 47, lilikutana mjini Geneva, Uswiss kwenye kikao chake cha pili, ambapo kulifanyika majadiliano ya wiki tatu mfululizo kusailia mada kadha wa kadha zinazoambatana na taratibu za kuboresha utekelezaji wa haki za kiutu ulimwenguni.

Umoja wa Mataifa waonya kuzuka hali ya hatari kieneo pindi Usomali itageuzwa kuwa jukwaa la vita vya wakala na mataifa jirani

Wiki hii Mwakilishi Maalumu wa KM juu ya Usomali, Francois Lonseny Fall alizuru Makao Makuu ya UM kushauriana na KM pamoja na Baraza la Usalama kuhusu hali iliyojiri Usomali karibuni.

Mukhtasari wa Mkutano Mkuu kusailia uharibifu wa hewa duniani

Mkutano wa 12 kwa Mataifa 189 Yalioridhia Mkataba wa Hifadhi Dhidi ya Uharibifu wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa pamoja na kuidhinisha Mkataba wa Kyoto ulianzishwa rasmi mwanzo wa juma mjini Nairobi, Kenya ambapo kulizingatiwa hatua za kudhibiti kipamoja athari za mabadiliko yaliyoletwa na uchafuzi wa hewa duniani.

Mahakama ya ICC yasikiliza kesi yake ya kwanza mjini Hague

Mahakama pekee ya kudumu ya kimataifa juu ya makosa ya jinai ya vita, yaani Mahakama ya ICC ilisikiliza kesi yake ya mwanzo Alkhamisi, Novemba tisa(2006), iliofanyika mjini Hague, Uholanzi inayohusika na Thomas Lubanga Dyilo, aliyekuwa jemadari wa kundi la wanamgambo wa kundi la Forces Patriotiques pour la Liberation du Congo (FPLC) katika wilaya ya Ituri, Mashariki-kaskazini ya JKK katika miaka ya 2002-03.

UNHCR imeanzisha ugawaji mkuu wa nguo kwa wahamiaji wa DRC kabla ya majira ya mvua kuwasili

Shirika la UM juu ya huduma za Wahamiaji (UNHCR) karibuni limeanzisha huduma za ugawaji wa nguo kwa wakimbizi 50,000 ziada muhitaji waliopo kwenye kambi za Gety na Kagaba, katika Jimbo la Ituri.

Shirikisho la Urusi kusaidia Kenya kukabilina na ukame

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limefadhiliwa msaada wa dharura wa dola milioni 2 kutoka Shirikisho la Urusi utakaotumiwa kwenye operesheni za kuwapatia chakula watu milioni 3 nchini Kenya, walioathirika na tatizo la ukame.

KM anaamini Afrika itafaidika kimaendeleo ikijifunza namna ya kupunguza ufukara kutoka kwa Wachina

KM wa UM Kofi Annan ameipongeza Uchina kwa kuahidi kuongeza, kwa mara mbili zaidi, misaada ya maendeleo kwa bara la Afrika itakapotimia 2009. Ahadi hii ilifikiwa na wawakilishi wa Serekali ya Uchina na viongozi wa Afrika waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Baraza la Ushirikiano wa Uchina na Afrika uliofanyika majuzi mjini Beijing.

Mshauri Mstaafu wa Misaada ya Dharura kuzuru Afrika kwa mara ya mwisho

Makamu KM juu ya Masuala ya Kiutu na Misaada ya Dharura, Jan Egeland wiki hii ameanza ziara ya mwisho ya siku 10 katika bara la Afrika kabla ya kustaafu mwisho wa mwaka.