Shaka na shuku zikiendelea kugonga vichwa vya wakazi wa dunia hii wakati huu wa kusambaa kwa virusi vya Corona, au COVID-19, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu ni wakati wa busara na sio kupagawa, wakati wa sayansi na sio unyanyapaa na zaidi ya yote ni wakati wa ukweli na si hofu.