Ulaya

Fifisha mwanga wa taa usiku ili kuokoa maisha ya ndege wanaohama duniani:UN 

Katika siku ya ndege wanaohama duniani Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuchukua hatua kufifisha nuru ya mwanga usiku ili kunusuru maisha ya mamilioni ya Ndege kila mwaka. 

Muungano mpya wazinduliwa kuhakikisha lishe bora kwa watoto na kila mtu: UN

Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO, la kuhudumia Watoto UNICEF, la mpango wa chakula duniani WFP na la mazingira UNEP leo yamezindua muungano mpya kwa lengo la kuchukua hatua ili kuhakikisha lishe bora kuanzia mifumo endelevu ya chakula kwa watoto na kila mtu. 

G7: FAO yatoa mapendekezo ya kukabiliana na uhaba wa chakula wa sasa na ujao

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO Qu Dongyu ametoa wito kwa nchi tajiri zaidi duniani G7 kusaidia kukabiliana na uhaba wa chakula katika siku zijazo kwani vita inayoendelea nchini Ukraine imepunguza usambazaji na kupandisha bei juu katika viwango vya kuvunja rekodi na kuyaweka mashakani mataifa ambayo tayari yana hatari ya kuathirika kote barani Afrika na Asia.

Siku ya kimataifa ya Afya ya mimea yaadhimishwa kwa mara ya kwanza 

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Afya ya Mimea, IDPH, ulimwengu ukiadhimisha siku hiyo kwa mara ya kwanza, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, limesema mabadiliko ya tabianchi na shughuli za binadamu zinabadilisha mifumo ikolojia na kuharibu bayonuai huku hali hiyo ikiunda maeneo mapya kwa ajili ya wadudu waharibifu kustawi.  

Wanawake na wasichana wakumbwa na ukatili wa kingono Ukraine

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Michelle Bachelet amesema ofisi yake imethibitisha matukio ya ukatili wa kingono dhidi ya wanawake nchini Ukraine, ambako mapigano yanaendelea tangu uvamizi uliofanywa na Urusi kuanzia tarehe 24 mwezi Februari mwaka huu.

Kampeni ya ‘Be Seen Be Heard’ yaani ‘Onekana Sikika’ yazinduliwa kuwapa sauti vijana ulimwenguni 

Vijana wana haki ya kujumuishwa katika maamuzi ya kisiasa yanayowahusu, hata hivyo, vikwazo vingi vinazuia ushiriki wao. 

Vita Ukraine vyapukutisha mamilioni ya ajira: ILO

Takribani ajira milioni 4.8 nchini Ukraine zimetokomea kufuatia uvamizi wa Urusi dhidi ya taifa hilo, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO katika ripoti yake iliyotolewa leo huko Geneva, Uswisi. 

Ukikutana na wakimbizi ni vigumu kutoguswa na simulizi zao- Guterres akiwa Moldova

Ni vigumu kukutana na wakimbizi halafu usiguswe na simulizi zao! Ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyotoa leo huko Chişinau, mji mkuu wa Moldova wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea kituo cha kuhifadhi wakimbizi kutoka Ukraine, kituo kilichoko mjini humo.

Pombe inaua mtu mmoja kila baada ya sekunde 10 : WHO

•    Ripoti ya WHO yafichua mbinu za ushawishi zinazotumiwa na kampuni za pombe
•    Mbinu hizo zinazidi udhibiti wa matangazo.
•    Watu mashuhuri mitandaoni watumika
•    Mbinu mpya zabuniwa kuwalenga wanawake

Shukrani Moldova kwa kufungulia wakimbizi milango licha ya changamoto- Guterres

Umoja wa Mataifa umesema uko na mshikamano na wananchi na taifa la Moldova kutokana na kitendo chake cha kufungua milango yake na kukaribisha raia takribani nusu milioni kutoka Ukraine wanaokimbia vita nchini mwao.