Mafanikio ya miongo kadha ya mgao wa chakula shuleni yaliyolenga watoto walio hatarini na wasio na uwezo wa kupata mlo bora, yako hatarini kutumbukia nyongo kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19, imesema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo huko Roma Italia ikimulika hali ya mpango wa mlo shuleni duniai, SOSFW.