Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya muungano wa ustaarabu, UNAOC Miguel Moratinos amelaani vikali kitendo cha kuchomwa kwa Quran Tukufu kilichofanywa na watu wenye misimamo mikali kwenye mji wa Malmo nchini Sweden.
Kamisheni ya Muungano wa Ulaya, EU leo imethibitisha nia yake ya kushiriki katika mfumo wa COVAX wa kusaka chanjo dhidi ya COVID-19 na itakayopatikana kwa watu wote na popote pale duniani.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 linapeleka mrama harakati za kupatikana kwa amani endelevu duniani.
Janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID- 19 likiendelea kuripotiwa maeneo mbalimbali duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa tamko lake la kisera lenye lengo la kuhakikisha kuwa janga hilo halizidishi pengo lililokuwa la walio na elimu na wasio na elimu.
Wiki ya unyonyeshaji duniani imeanza Agosti Mosi huku Umoja wa Mataifa ukizitaka jamii zote kila mahali “kuunga mkono unyonyeshaji kwa ajili ya kuwa na dunia yenye afya.”
Kamati ya dharura ya shirika la afya duniani WHO ya kupambana na janga la corona au COVID-19 imekutana mjini Geneva Uswis katika kikao maalum kilichoitishwa na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus.