Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la idadi ya watu duniani UNFPA imesema ili kukabiliana na janga la kimyakimya la mila potofu hatua za haraka zinahitajika kukomesha ukeketaji (FGM), ndoa za utotoni na mila zingine ambazo zinathiri wanawake na wasichana.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalopambana na ukimwi UNAIDS Winnie Byanyima amesema janga la corona au COVID-19 limeongeza adha kwa watu wanaoishi na VVU lakini pia kuyumbisha uchumi wa dunia na kuongeza pengo la usawa wa kijinsia, hivyo ameisihi dunia kuchukua hatua zinaozingatia haki za binadamu kama njia pekee ya kulidhibiti janga hilo.
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya biashara ndogo na za kati, SMEs, Umoja wa Mataifa unataka hatua zaidi zichukuliwa kusaidia sekta hii kwa kuwa imeathirika zaidi wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.
Utesaji ni ukatili mbaya sana wa haki za binadamu amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio guterres hii le ikiwa ni siku ya kimataifa ya kuwaunga mkono waathirika wa utesaji.
Katiba ya Umoja wa Mataifa ambayo ilipitishwa na kutiwa Saini 26 Juni 1945 mjini San Francisco nchini Marekani na mataifa 50, leo inasherehekea miaka 75.
Ujerumani na Ufaransa leo zimesisitiza uungaji mkono wa kisiasa na kifedha kwa shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO wakati huu ambapo janga la virusi vya Corona au COVID-19, limeendelea kutikisa ulimwengu.
Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, nchi waangalizi na wengineo wametuma ujumbe mzito wa kisiasa wiki hii kwa kutangaza kwamba sahihi 170 sasa zimeidhinisha wito wa Umoja wa Mataifa wa kunyamazisha silaha na kusimama Pamoja dhidi ya tishio la kimataifa la janga la virusi vya corona au CIVID-19.
Katiba ya Umoja wa Mataifa ikiwa inaelekea kutimiza miaka 75 juma hili Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterrres amesema changamoto lukuki zinazoikabili dunia hivi sasa zinahitaji mwongozo ili kuzitatua na mwongozo huo ni katiba ya Umoja wa Mataifa.
Wakati dunia ikiendelea kupambana na janga la corona au COVID-19 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amewaenzi watumizi wa umma walio mstari wa mbele katika kupambana na janga hili na pia kwa huduma yao ya muhimu kwa binadamu.
Ikiwa leo ni siku ya wajane duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka kuangaziwa zaidi kwa kundi linalosahaulika mara kwa mara, wajane, hususan wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.