Jumamosi ya leo, Shirika la afya ulimwenguni limethibitisha kupitia ofisi yake ya kanda ya ulaya kuwa virusi vya Corona au 2019-nCoV ambavyo kwa majuma kadhaa sasa vimesababisha madhara makubwa nchini China, sasa vimethibitika nchini Ufaransa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia hivi sasa iko katika hali ya taharuki na sintofahamu ikikabiliwa na mambo makubwa manne ambayo yanatishia mustakbali wa mamilioni ya watu na sayari yenyewe.
Kuna aina mbalimbali za sigara za kielektroniki kwa kiingereza Electronic Nicotine Delivery Systems au (ENDS), zikiwa na kiwango mbalimbali cha kichangamsho aina ya Nicotine na moshi hatarishi.
Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa,FAO litaimarisha uwezo wa mfumo wake wa ufuatiliaji wa misitu ulimwenguni na hii ni kutokana na ushirikiano wake mpya na shirika la anga za juu la Japan, JAXA.
Pengo la usawa duniani linaongezeka kwa zaidi ya asilimia 70 ya watu wote duniani na hivyo kuongeza hatari ya migawanyiko na kuathiri maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Lakini ongezeko hilo linaweza kudhibitiwa na kushughulikiwa katika ngazi ya kitaifa na kimataifa kwa mujibu wa ripoti ya utafiti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo Jumanne.
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limezindua jukwaa la kihistoria la kidijitali HungerMapLIVE, ambalo litakusanya takwimu muhimu kuhusu hali ya uhakika wa chakula katika nchi zaidi ya 90 duniani.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kutokomeza Ukimwi, UNAIDS linatoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa haki ya afya kwa wote inazingatiwa kwa kupatia kipaumbele uwekezaji wa umma katika sekta ya afya.
Takribani nusu ya watu bilioni moja wanafanya kazi saa chache za kulipwa kuliko zile ambazo wangependa au kukosekana kabisa kwa kazi za kulipwa. Hiyo ni kwa mujibu wa riupoti mpya ya shirika la kazi duniani.