Mamilioni ya magari yaliyokwisha kutumiwa, ambayo yameuzwa katika nchi zinazoendelea, hayafai, yana ubora wa chini na yanachangia kwa kiasi kikubwa katika uchafuzi wa hewa na hivyo kutatiza juhudi za kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, imesema ripoti mpya ya Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP.