Wakati huu dunia ikiendelea kuhaha kuhakikisha chanjo dhidi ya corona au COVID-19 iliyokwishapatikana inasambazwa kwa kila mkazi wa dunia, shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limefafanua kuhusu chanjo na jinsi zinavyotengenezwa.
Idadi ya watoto wa shule walioathiriwa na kufungwa kwa shule kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 imeongezeka kwa asilimia 38 mwezi uliopita wa Novemba, hali hiyo ikiweka mkwamo mkubwa kwenye maendeleo ya masomo na ustawi wa wanafunzi zaidi ya milioni 90 ulimwenguni, limeeleza shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wafanyakazi wa kujitolea, Umoja wa Mataifa umetumia siku hii adhimu kuangazia wafanyakazi wa kujitolea na mchango wao katika kukabiliana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona au COVID-19.
Janga la ugonjwa wa Corona, COVID-19 likiendelea kutikisa duniani, Umoja wa Mataifa hii leo umeanza kikao maalum cha ngazi ya juu cha siku mbili kujadili janga hilo ambalo hadi sasa limesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,400,000 duniani kote.
Kufuatia mapendekezo ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO ya faida za kitabibu zinazotokana na zao la bangi kwa afya , nchi 27 wanachama wa tume ya Umoja wa Mataifa ya dawa za kulevya wamepiga kura kuunga mkono kuondoa bangi katika orodha ya dawa hatari za kulevya katika maamuzi ambayo pia yalipingwa kwa kura 25 na mjumbe mmoja kutopiga kura.
Ripoti mbili kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa zilizotolewa hii leo, kwa namna tofauti zimeonesha namna athari za ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona, zikavyosababisha kuporomoka kwa nguvu ya uchumi ya watu wengi na hivyo kuwaingiza katika umaskini uliokithiri.
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa amesema wakati dunia ikijikwamua kutoka kwenye janga la COVID-19 ni lazima kuhakikisha kwamba matarajio na haki za watu wenye ulemavu zinajumuishwa na hilo litatimia tu endapo watu hao watashirikishwa na kuwakilishwa ipasavyo.
Nchi kadhaa hivi karibuni zimetangaza ahadi za kupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wao wa hewa ukaa, na kuitokomeza kabisa hewa hiyo katika miaka ijayo. Tamko hilo limekuwa kilio cha kimataifa, kinachotajwa mara kwa mara kama hatua muhimu ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi, na uharibifu yanaousababisha.
Katika kuadhimisha siku ya kimataifa kwa ajili ya kutokomezwa utumwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameainisha athari za mifumo ya kisasa ya utumwa na kusisitiza kwamba vitendo hivyo vilivyopitwa na wakati havina nafasi katika karne ya 21.