Ulaya

Hatimaye meli yenye shehena ya ngano yaondoka Ukraine kuelekea Pembe ya Afrika

Meli ya kwanza ya Ukraine yenye na unga wa ngano wa Ukraine utakaosambazwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP kwenye operesheni zake za kibinadamu imeondoka bandari ya Yuzhny nchini Ukraine hii leo,  hatua ambayo imetajwa kuwa ya muhimu zaidi na inayohitajika ya kuondoa nafaka kwenye taifa hilo lenye mzozo kuelekea nchi zinazokumbwa na janga la uhaba wa chakula duniani. 

Watoto walioathiriwa na migogoro hawawezi kusubiri elimu yao

Kutoka Ethiopia hadi Chad na Palestina, Elimu haiwezi kusubiri au ECW , ni mradi wa Umoja wa Mataifa wa elimu katika maeneo yenye dharura na migogoro ya muda mrefu, ambao umesaidia mamilioni ya wavulana na wasichana walioathiriwa na migogoro duniani kote kutimiza ndoto zao.

Zaidi ya wahudumu wa kibinadamu 140 waliuawa mwaka jana, wengi wao wa kitaifa

Kuelekea siku ya usaidizi wa kibinadamu duniani tarehe 19 mwezi huu wa Agosti, Umoja wa Mataifa leo umesema kadri majanga yanavyozidi kuongezeka duniani maisha ya watoa misaada yako hatarini zaidi na kwamba mwaka jana pekee wa 2021 wahudumu zaidi ya 140 wa kiutu waliuawa duniani kote.

Vizazi vyote tuungane kuwasaidia vijana : Guterres

Ikiwa leo ni siku ya vijana duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa jamii kuwasaidia vijana kwa kuwekeza kwenye kuwapatia elimu na kuwajengea uwezo wa kiujuzi kupitia mikutano pamoja na kufanya mabadiliko katika mifumo ya elimu.

Umoja wa Mataifa wataka kusitishwa mapigano karibu na kiwanda cha nyuklia nchini Ukriane

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza kuwa na wasiwasi mkubwa kwa hali inayoendelea ya mapigano ndani na karibu na kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia kilichoko kusini mwa nchi ya Ukriane. 

Ajira kwa vijana duniani inasuasua; hali ngumu zaidi kwa vijana wa kike- ILO

Suala la vijana kupata ajira tena kujikwamua kutoka hali ngumu ya maisha baada ya janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 limeendelea kusuasua, imesema ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO iliyotolewa leo kuelekea siku ya vijana hapo kesho, ambapo shirika hilo linasema hali hiyo inathibitisha kuwa COVID-19 iliathiri zaidi vijana kuliko marika mengine, vijana wa kike wakiathirika zaidi.
 

Cryptocurrency: UNCTAD yatangaza sera 3 zakufuatwa katika matumizi ya sarafu za kidijitali

Kamati ya  Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo UNCTAD imetoa mapendekezo ya sera tatu zinazoweza kutumiwa na nchi zinazoendelea kufuatia kuongezeka kwa matumizi ya sarafu za kidijitali au Cryptocurrency wakati huu ambapo nchi nyingi hazina sera wala mifumo madhubuti ya udhibiti na matumizi yake kwa jamii.

WMO: Mwezi Julai ulirekodi joto kali, Ukame na Moto wa nyika kwa wakati mmoja

Huku kukiwa na joto kali, ukame na moto wa nyika, sehemu nyingi za dunia zilikuwa zimepitia mojawapo ya Julai tatu zenye joto zaidi katika rekodi, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa WMO hii leo.

Mashine za kusaidia watoto kupumua zapelekwa Ukraine; ni ubunifu kutoka Kenya

Mashine 220 za kusaidia watoto wachanga kupata hewa ya oksijeni kutokana na kuwa hatarini kufariki dunia baada ya kuzaliwa ambazo zimetengenezwa nchini Kenya kwa msaada wa shirika la Umoja wa MAtaifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa na tiba kwa gharama nafuu UNITAID zimepelekwa nchini Ukraine wakati huu ambapo vita vinakwamisha huduma za uzazi na kujifungua. 

Bei za vyakula zashuka katika soko la dunia kwa mwezi Julai

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO hii leo limetangaza bei za vyakula zilishuka kwa kiasi kikubwa mwezi Julai,2022 na kuashiria kushuka kwa mwezi wa nne mfululizo tangu zilipoweka rekodi ya juu zaidi mwanzoni mwa mwaka kufuatia vita ya Ukraine.