Ni lazima Vatican ichukue hatua kuhakikisha haki kwa watu ambao walinyanyaswa kingono na watawa walipokuwa watoto amesema mtaalam huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Alhamisi.
Shirika la afya ulimwenguni, WHO linakadiria kwa mara ya kwanza kwamba idadi ya wanaume wanaotumia tumbaku imepungua ikiashiria mabadliko katika janga la tumbaku kimataifa.
Mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu kuhusu wakimbizi umefunga pazia huko Geneva, Uswisi ukiwa na ahadi lukuki za kusaidia wakimbizi na jamii zinazowahifadhi huku ahadi nyingi zaidi zikijikita katika usaidizi wa muda mrefu hususan ujumuishaji.
Hatimaye nuru imeangazia wagonjwa wa saratani ya titi husasan katika nchi za kipato cha chini baada ya shirika la afya duniani WHO hii leo kuidhinisha kutengenezwa kwa dawa ya mfanano ya gharama nafuu iitwayo TRASTUZUMAB.
Tatizo la wakimbizi ni jukumu la kila mtu sio wakimbizi au nchi zinazowahifadhi pekee, kwani nimejifunza ukarimu sio lazima uendane na utajiri. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hii leo katika kongamano la kimatifa kwa ajili ya wakimbizi linaloendelea mjini Geneva Uswis.
Zaidi ya nchi 1 kati ya 3 za kipato cha wastani na kipato cha chini zinakabiliwa na changamoto kubwa mbili za kiafya , utipwatiwa na lishe dunia kutokana na mabadiliko katika mifumo ya chakula imesema ripoti mpya ya shirika la afya duniani WHO iliyochapishwa leo kwenye jarida la kimataifa la afya The Lancet.
Hii leo kwenye makao makuu ya shirika la afya duniani, WHO huko Geneva, Uswisi kumefanyika tukio maalum la kuadhimisha miaka 40 tangu kutokomezwa kwa ugonjwa wa ndui.
Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifai wameipongeza serikli ya Ugiriki kwa hatua kubwa katika mchakato wa kukomesha kuweka watu kizuizini lakini bado ina changamoto kubwa kutokana na kusambaa kwa vitendo vya kusweka watu vizuizini katika mfumo wa haki na uhalifu na mifumo ya uhamiaji ambayo lazima imalizike.
Nchini Ujerumani mafunzo mahsusi yanayotolewa na kampuni za kijerumani kwa wakimbizi yameleta siyo tu matumaini kwa wakimbizi bali pia kusaidia kujenga utangamano na jamii zinazowazunguka.