“Leo, tunayo heshima ya kuwaenzi wanawake na wanaume zaidi ya milioni moja ambao wameshiriki kama walinda amani wa Umoja wa Mataifa tangu mwaka 1948.” Ndivyo alivyoanza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya walinda amani.