Janga la COVID-19 limekuwa na athari kubwa kwa afya ya akili ulimwenguni kote, na lazima hatua zichukuliwe ili "kukomesha ukosefu wa usawa uliofichuliwa na janga hilo", pamoja na upatikanaji wa huduma muhimu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya akili, inayoadhimishwa leo Jumapili Oktoba 10.