Mtaalamu maalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Agnès Callamard amesema kanuni za ulinzi wa ndege za kiraia zinazoruka kwenye maeneo ya mizozo ya kijeshi zisiwe na utata wowote na ziwe wazi ili kulinda maisha ya abira na wafanyakazi wa ndege hizo.
Umoja wa Mataifa unaadhimisha siku ya nukta nundu duniani Jumatatu Januari 4, kwa kusisitiza umuhimu wa mfumo huu wa kupitisha habari kwa ajili ya kuhakikisha haki za watu wenye ulemavu wa kutoona na watu wenye uoni hafifu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelrezea huzuni yake kufuatia kifo cha afisa wa zamani wa ngazi ya juu kwenye umoja wa Mataifa Brian Urquhart aliyeutumikia Umoja wa Mataifa kwa miaka zaidi ya 40.