Kampeni mpya iliyozinduliwa mwezi huu wa Desemba na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani linalohusika pia na afya ya uzazi UNFPA ya “Hakimiliki ya miwli wa binadamu” ina lengo la kuwasukuma watunga sera, sekta za teknolojia na mitandao yote ya kijamii kuuchukulia unyanyasaji na ukatili wa miili ya binadamu hususani ya wanawake mtandaoni kuwa ni suala linalohitaji kupewa uzito kama ilivyo ukiukwaji wa hakimiliki zingine. Flora Nducha na taarifa kamili