Ulaya

Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu unaathiri watu milioni 50 kote ulimwenguni, WHO yatoa mwongozo wa kupunguza hatari

Shirika la afya ulimwenguni WHO leo limetoa mwongozo mpya wa kusaidia watu kupunguza hatari za ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, ambao pamoja na mambo mengine unataja masuala kama vile kufanya mazoezi mara kwa mara, kutovuta sigara, kuepuka matumizi hatarishi ya vileo na lishe bora.

Kuhusu majanga ni hali ya usipoziba ufa utajenga ukuta -ripoti ya FAO

Wakulima maskini wanaweza kupata faida za kiuchumi na faida zingine kwa kutekeleza mifumo bora ya kilimo inayolenga kuimarisha uwezo wao katika kukabiliana na majanga na misukosuko ya asili, imesema ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO iliyotolewa leo.

Heko vijana wa New Zealand, dunia tuzingatie mambo manne katika mabadiliko ya tabianchi- Guterres

Vijana nchini New Zealand wamepongezwa na Umoja wa Mataifa kwa kazi nzuri na mchango wao mkubwa katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi , huku wakiaswa kuongeza juhudi na kuwa wabunifu Zaidi kwa kusaka suluhu mbadala kwa ajili ya changamoto hii inayoighubika duniani.

Watu mashuhuri 6 wajumuishwa kwenye jopo la wachechemuzi wa SDGs

Wakati Umoja wa  Mataifa na wadau wake duniani kote wanahaha kusongesha na kufanisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ifikapo mwaka 2030, wajumbe wengine wapya 6 wenye ushawishi wamejumuishwa kwenye bodi ya watetezi wa SDGs hii leo na kuahidi kusongesha malengo hayo kwa niaba ya amani, ustawi, wakazi wa Dunia na ubia.

Gharama ya uagizaji chakula kupungua 2019, lakini Afrika haitonufaika

Gharama ya uagizaji wa chakula duniani kwa mwaka huu wa 2019 itapungua kutokana na ongezeko la uzalishaji wa bidhaa, imesema ripoti mpya ya makadirio ya chakula iliyotolewa leo na shirika la chakula duniani, FAO.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa waitaka Iran imwachie huru mwanazuoni Xiyue Wang.

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wameisihi Iran imwachie haraka mwanazuoni Xiyue Wang wakidai kushikiliwa kwake kinyume cha utaratibu kwa takribani miaka mitatu ni ukiukwaji wa wazi wa haki za binadamu chini ya sheria za kimataifa.

UN  yazindua mpango wa kudhibiti ugaidi kwa kufuatilia taarifa za wasafiri

Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya kukabiliana na ugaidi, UNOCT leo umezindua mpango wa kudhibiti ugaidi kwa kufuatilia wasafiri.

Wabunifu sekta ya kilimo na chakula wabonga bongo Italia kusaidia kutokomeza njaa

Mkutano wa tano wa kimataifa kuhusu ubunifu kwenye sekta ya chakula na kilimo umeingia siku ya pili hii leo huko Milano nchini Italia ukichambua teknolojia bunifu zinazoweza kusaidia kutokomeza njaa duniani ifikapo mwaka 2030.

Watu 7400 hung’atwa na nyoka kila siku, WHO yachukua hatua

Je wajua kuwa watu 7400 hung’atwa na nyoka kila siku duniani kote na kati yao hao 220 hadi 380 hupoteza maisha?

Aina milioni 1 ya viumbe hatarini kutoweka-  Ripoti

Ripoti mpya kuhusu madhara ya shughuli za binadamu kwa mazingira inaonesha kuwa takribani aina milioni moja ya viumbe viko hatarini kutoweka ndani ya miongo kadhaa iwapo juhudi za sasa za kuhifadhi mazingira zitakwama.