COVID-19 imebadili maisha yetu na kuutumbukiza ulimwengu katika mateso na huzuni. Ndivyo alivyoanza ujumbe wake wa mwaka mpya 2020, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ujumbe alioutoa kwa njia ya video kutoka jijini New York, Marekani, makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
Ikiwa leo ni siku ya wahamiaji duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema ni mwaka wa kutathmini jinsi janga la Corona au COVID-19 lilivyosababisha mamilioni ya watu kukumbwa na machungu ya kutengana na familia zao na kutokuwa na uhakika wa ajira, jambo ambalo limewapatia watu hisia halisi ambazo wahamiaji hukumbana nazo kila wakati kwenye maisha yao.
Wakuu wa nchi na serikali mbalimbali 77 wameungana na viongozi wa makampuni ya biashara na kutana leo Jumamosi kwa njia ya mtandao kuzungumzia malengo na matamanio ya mabadiliko ya tabianchi na ahadi mpya za kuyatimiza.
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wafanyakazi wa kujitolea, Umoja wa Mataifa umetumia siku hii adhimu kuangazia wafanyakazi wa kujitolea na mchango wao katika kukabiliana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona au COVID-19.
Janga la ugonjwa wa Corona, COVID-19 likiendelea kutikisa duniani, Umoja wa Mataifa hii leo umeanza kikao maalum cha ngazi ya juu cha siku mbili kujadili janga hilo ambalo hadi sasa limesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,400,000 duniani kote.