Kuelekea maadhimisho ya miaka 75 ya Umoja wa Mataifa mwakani 2020, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres hii leo ametangaza kuwa maadhimisho hayo yatajumuisha mjadala jumuishi wa dhima ya jukumu la ushirikiano wa kimataifa katika kujenga mustakabali utakiwao ulimwenguni.
Amani, usalama, upendo na mshikamano ndio msingi wa mustakabali wa dunia, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku ya Umoja wa Mataifa hii leo.
Ikiwa leo ni siku ya chakula duniani wito ukiwa ni kutokomeza njaa- na kuwa na dunia ambako chakula chenye lishe bora kinapatikana kwa bei nafuu na kwa watu wote na kila mahali, Umoja wa Mataifa unahoji iweje leo hii zaidi ya watu milioni 820 hawana chakula cha kutosheleza mahitaji yao.
Baada ya mkutano wa ngazi ya juu kuhusu hatua kwa tabianchi uliotanguliwa na harakati za vijana kutaka hatua, Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa Antonio Guterres aliweka tafakuri yake kwenye tahariri iliyochapishwa na ubia wa vyombo vya habari 170 wenye wasomaji zaidi ya mamilioni.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ameziandikia barua nchi wanachama kuhusu ukata mbaya zaidi kuwahi kukabili chombo hicho chenye wanachama 193 kwa karibu muongo mmoja.
Suala la ulinzi wa wakimbizi ni moja ya vipaumbele vya awali kabisa vya Umoja wa Mataifa takriban miongo saba iliyopita hata hivyo, ufurushwaji wa watu bado unazua wasiwasi mkubwa kimataifa. Taarifa kamili na Arnold Kayanda
Ikiwa leo ni siku ya walimu duniani, viongozi wa mashirika manne ya Umoja wa Mataifa na wadau wake wametaka hatua za makusudi zichukuliwe ili kuvutia vijana kwenye tasnia hiyo adhimu.