Umoja wa Mataifa leo umezindua leo ripoti yake ya kimataifa kuhusu vijana, ikisema ushirikiswhwaji wa vijana bilioni 1.2 wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24 ni muhimu katika kufanikisha jamii endelevu, jumuishi na thabiti.
Ajira za viwango duni ni moja ya changamoto kubwa katika soko la ajira huku mamilioni ya watu wakilazimika kukubali mazingira duni ya kazi, kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO iliyotolewa leo.
Kufuatia ukweli ya kwamba lugha 600 za kiasili hupotea kila baada ya wiki mbili, Umoja wa Mataifa hii leo kwenye makao yake makuu mjini New York, Marekani umezindua rasmi mwaka wa kimataifa wa lugha hizo.