Hii leo huko Paris, Ufaransa, shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO linazindua rasmi mwaka huu wa 2019 kuwa mwaka wa kimataifa wa lugha za asili, kufuatia azimio lililopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2016.