Tuko hapa kutafakari tumefikia wapi hadi sasa katika mchakato wa kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs amesema rais wa Baraza la kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa-ECOSOC, Marie Chatardova jijini New York, Marekani hii leo wakati akifungua mkutano wa ngazi ya juu wa kutathmini malengo hayo.