Jijini New York Marekani hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameungana na viongozi wengine wa dini na wakazi wa jiji hilo kukumbuka watu 11 waliopoteza maisha katika shambulio la mwishoni mwa wiki kwenye sinagogi moja huko Pittsburg, jimboni Pennyslvania nchini Marekani.
Hatimaye watafiti wametegua kitendawili cha mioto aina ya uyoga au kuvu inayomeng’enyua plastiki na hivyo kuweka matumaini katika juhudi za kuondokana na plastiki zinazoharibu mazingira.
Leo ni siku ya miji duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake alioutoa kuiadhimisha siku hii, ametoa wito kwa dunia nzima kufanya kazi pamoja kujenga miji endelevu na stahimilivu ambayo inawapatia watu wote usalama na fursa. Taarifa zaidi na John Kibego
Zaidi ya asilimia 90 ya watoto duniani kote walio na umri wa chini ya miaka 15 huvuta hewa chafu kila siku ambayo inaweka maisha yao hatarini na wengi wao hufariki dunia imesema ripoti ya shirika la afya dunaini WHO.
Haki ya uhuru wa dini au imani ni suala mtambuka ambalo mara nyingi halieleweki vyema na kusababisha haki hiyo kukiukwa kwa kiasi kikubwa kote duniani.
Ufadhili wa sekta za umma pekee hautoshi kutimiza malengo ya maendeleo endelevu au SDG’s hivyo taasisi za maendeleo za kimataifa na za ufadhili lazima zishirikiane kujumuisha uwekezaji kutoka sekta binafsi.
Mkutano wa kimataifa kuhusu takwimu umeanza leo huko Dubai, Falme za Kiarabu ambapo Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed amesema mafanikio ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanategemea uwepo wa takwimu sahihi na za kutosha.
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya idadi ya watu imeonyesha bayana uhusiano mkubwa kati ya idadi ya watoto na na fursa ya mtu kupata haki ya msingi ya huduma za afya ya uzazi.