Baada ya mashauriano ya muda mrefu, hatimaye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeridhia mapendekezo ya marekebisho ya mfumo wa maendeleo wa chombo hicho chenye wanachama 193. Marekebisho hayo yanalenga kusogeza zaidi UN kwa wananchi wa kawaida ili hatimaye maendeleo yawe dhahiri ya watu na si vitu.
Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yamekubaliana kuanzisha mkakati maalum wa pamoja utakaosaidia kudhibiti athari za kiafya zinazosababishwa na mazingira duni.
Katika ulimwengu wa sasa unaoshuhudia migawanyiko, hofu ya vita vya nyuklia na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, Umoja wa Mataifa umeusihi ushirikiano zaidi na umoja miongoni mwa wanachama wa Muungano wa Ulaya, EU.
Watoto, wakati wote, wanahitaji amani na ulinzi, hiyo ni kauli iliyotolewa leo jijini New York, Marekani na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto la UNICEF, Henrietta H. Fore.
Maboya yamekuwa yanatumika kusafirishia wakimbizi na wasaka hifadhi. Mara nyingi maboya haya yanapotia nanga huko Ulaya huwa yamechakaa na hivyo kutupwa kiholela. Hivi sasa wasichaan wawili huko Ujerumani wamegeuza taka hizo kuwa bidhaa ya aina yake.
Idadi ya watoto wanaokosa kunyonya maziwa ya mama bado ni kubwa hususan miongoni mwa nchi tajiri duniani umesema uchambuzi mpya uliotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.