Nchini Yemen, muhula mpya wa shule ukianza huku mzozo ukiendelea, watoto milioni 2 hawawezi kwenda shule, idadi ikijumuisha nusu milioni ambao ni watoro wa shule tangu mzozo uanze nchini humo mwaka 2015.
Leo katika ufunguzi wa mkutano wa ngazi ya juu wa viongozi wa Umoja wa Mataifa kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutrerres amesema hatakuwa mtamazaji aliye kimya kwa uhalifu ambao unaathiri hali ya sasa na kuharibu haki kwa vizazi vijavyo kwa ajili ya mustakabali endelevu akiongeza kwamba viongozi wana haki ya kufanya kila wawezalo kukomesha janga la mabadiliko ya tabianchi kabla halijatukomesha.
Nchi ni lazima ziongeze matumizi kwenye huduma za kimsingi za afya kwa takriban asiliamia 1 ya pato loa la kitaifa ikiwa dunia inataka kupunguza mianya ya kutimiza malengo ya afya ifikapo mwaka 2015, kwa mujibu wa ripoti mpya kutoka kwa Shirika la Afya Duniani na washirika kabla ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa huduma za afya zilizo muhimu.
Kuelekea siku ya kimataifa ya amani ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 21, leo katika maadhimisho kwenye Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres ametoa wito wa hatua madhubuti kuchukuliwa kukabiliana na changamoto kubwa za dunia ikiwemo mabadiliko ya tabianchi ili kudumisha amani kwa wote.
Tukielekea wiki ya vikao vya mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa vitakavyowakutanisha viongozi wa dunia katika makao makuu ya umoja huo mjini New York Marekani kuanzia jumatatu ya wiki ijayo, Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Modest Mero amezungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na kueleza kuwa mijadala ya viongozi wakuu wa dunia itatawaliwa na changamoto kuu tano ambazo dunia nzima inakabiliana nazo hivi sasa.
Wanawake zaidi na watoto wao kwa sasa wanaishi zaidi ya hapo awali kulingana na makadirio mapya ya watoto wanaokufa wakati wa kuzaliwa au kina mama wanaofariki dunia wakati wa kujifungua . Makadirio hayo yametolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la kuhudumia Watoto duniani UNICEF na Shirika la Afya Duniani WHO.
Mamilioni ya watu wanaathiriwa kila mwaka kutokana na huduma za afya zisizo salama kote duniani, hali inayosababisha vifo vya watu milioni 2.6 kwenye nchi za kipato cha chini na zile za kipato cha wastani.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema dunia inapojikita katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi basi isipuuze tabaka la Ozoni na kuwa na tahadhari ya tishio kubwa linalosababishwa na matumizi haramu ya gesi zinazotoboa tabaka la Ozoni au chlorofluorocarbons.“utambuzi wa hivi karibuni wa utoaji wa moja ya gesi hizo (CFC-11) unatukumbusha kwamba tunahitaji kuendelea na mifumo ya kufuatilia , kutoa taarifa, kuboresha na kuchukua hatua.”
Mamia ya maelfu ya raia wa Venezuela wanaendelea kuweka maisha yao rehani na kufanya safari za hatari ili kukwepa hali ngumu ya maisha nchini mwao na kukimbilia nchini jirani ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linashirikiana na nchi mwenyeji kuwasaidia.