Mkutano wa jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu maendeleo endelevu, SDGs ukiendelea hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani, imeelezwa kuwa ushiriki wa vijana katika kufanikisha malengo hayo sio suala la mjadala kwani ni lazima kundi hilo lishiriki kikamilifu ili malengo hayo yafanikishwe ifikapo mwaka 2030.