Ulaya

Magonjwa yatokanyo na matumizi ya tumbaku yanagharimu dunia dola trilioni 1.4- WHO

Gharama za magonjwa yatokanayo na matumizi ya tumbaku kila mwaka ni dola trilioni 1.4 kote ulimwenguni kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la afya duniani, WHO iliyotolewa leo Mei 31 kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku.

Ushindi wa tuzo ya Charlemangne ni heshima kubwa kwangu na UN- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amepokea tuzo ya Charlemangne huko mjini Aachen nchini Ujerumani na kusema kuwa ni heshima kubwa sana kwake.

Azimio lapitishwa Geneva kuhusu uwazi wa bei za dawa

Mkutano wa Baraza Kuu la shirika la afya duniani, WHO umefikia ukingoni leo kwa kupitisha azimio linalohusu kuboresha suala la uwazi wa masoko ya dawa, chanjo na bidhaa nyingine za afya katika jitihada za uwezekano katika kurahisisha upatikanaji bidhaa hizo. 

Wanawake katika uongozi huleta utendaji bora wa biashara.

Ripoti mpya ya shirika la kazi duniani, ILO imeonesha kuwa kampuni za kibiashara zenye uongozi wa ngazi ya juu ulio na mchanganyiko mzuri wa jinsia ya wanawake na wanaume zinapata faida kubwa. 

Dunia bila nyuki ni zahma kwa mustakabali wa chakula:FAO

Leo ni siku ya nyuki duniani siku ambayo inatanabaisha umuhimu wa nyuki na tishio linalowakabili viumbe hao, kutoweka kwao utakuwa mtihani mkubwa kwa dunia  limesema shirika la chakula na kilimo FAO  hususani kwa mustakabali wa chakula .

Mtoto 1 kati ya 7 duniani kote huzaliwa na uzito mdogo kupindukia- Ripoti

Takwimu mpya zilizotolewa leo na watafiti kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa na Chuo cha tiba za kitropiki na afya cha London, Uingereza zimeonyesha kuwa mwaka 2015 zaidi ya watoto milioni 20 walizaliwa duniani kote wakiwa na uzito wa chini kupindukia, ambao ni chini ya kilo mbili na nusu au pauni 5.5

Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu unaathiri watu milioni 50 kote ulimwenguni, WHO yatoa mwongozo wa kupunguza hatari

Shirika la afya ulimwenguni WHO leo limetoa mwongozo mpya wa kusaidia watu kupunguza hatari za ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, ambao pamoja na mambo mengine unataja masuala kama vile kufanya mazoezi mara kwa mara, kutovuta sigara, kuepuka matumizi hatarishi ya vileo na lishe bora.

Heko vijana wa New Zealand, dunia tuzingatie mambo manne katika mabadiliko ya tabianchi- Guterres

Vijana nchini New Zealand wamepongezwa na Umoja wa Mataifa kwa kazi nzuri na mchango wao mkubwa katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi , huku wakiaswa kuongeza juhudi na kuwa wabunifu Zaidi kwa kusaka suluhu mbadala kwa ajili ya changamoto hii inayoighubika duniani.

Wabunifu sekta ya kilimo na chakula wabonga bongo Italia kusaidia kutokomeza njaa

Mkutano wa tano wa kimataifa kuhusu ubunifu kwenye sekta ya chakula na kilimo umeingia siku ya pili hii leo huko Milano nchini Italia ukichambua teknolojia bunifu zinazoweza kusaidia kutokomeza njaa duniani ifikapo mwaka 2030.

Tunahitaji dunia isiyo na vifo na majeruhi wa ajali za barabarani:WHO

Maadhimisho ya tano ya kimataifa ya wiki ya Umoja wa Mataifa ya usalama barabarani yameanza leo na maelfu ya wanaharakati duniani kote wakichagiza haja ya kuwa na uongozi thabiti kwa ajili ya kuokoa na kulinda maisha ya watu barabarani.