Umoja wa Mataifa umeisihi dunia kushikamana na wakimbizi ambao wamelazimika kufungasha virago kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vita, mauaji , njaa na hata mateso kwani wanachokitaka ni amani.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limemchagua mwanadiplomasia na mwanazuoni kutoka Nigeria Tijjani Mohammad Bande kuwa rais wa mkutano wa 74 wa baraza hilo utakaoanza mwezi Septemba mwaka huu hadi Septemba mwakani.