Amani, usalama, upendo na mshikamano ndio msingi wa mustakabali wa dunia, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku ya Umoja wa Mataifa hii leo.
Ikiwa leo ni siku ya chakula duniani wito ukiwa ni kutokomeza njaa- na kuwa na dunia ambako chakula chenye lishe bora kinapatikana kwa bei nafuu na kwa watu wote na kila mahali, Umoja wa Mataifa unahoji iweje leo hii zaidi ya watu milioni 820 hawana chakula cha kutosheleza mahitaji yao.
Suala la ulinzi wa wakimbizi ni moja ya vipaumbele vya awali kabisa vya Umoja wa Mataifa takriban miongo saba iliyopita hata hivyo, ufurushwaji wa watu bado unazua wasiwasi mkubwa kimataifa. Taarifa kamili na Arnold Kayanda