Katika siku ya afya duniani hii leo, Umoja wa Mataifa unaendelea kupigia chepuo haki ya msingi ya kila mtu kupata huduma ya afya popote pale alipo. Umaskini unaongezewa kasi kwani watu wanatumia fedha nyingi kwenye matibabu.
Siku ya Jumamosi ya tarehe 7 Aprili mwaka huu wa 2018 ni kumbukizi ya kimataifa kuhusu mauaji ya kimbari nchini Rwanda. Umoja wa Mataifa ulitangaza rasmi mwanzoni mwa mwaka huu siku hii kutambuliwa kimataifa.
Kila uchao manyanyaso wapatayo wahamiaji yanaripotiwa kila kona ya dunia, na sasa Umoja wa Mataifa pamoja na Muungano wa Ulaya wameamua kuchukua hatua.