Janga la mlipuko wa virusi vya corona au COVID-19 limefanya macho yote ya Dunia kuelekezwa kwenye mtihani huu mkubwa zaidi ambao ulimwengu umekumbana nao tangu Vita vya Pili vya Dunia amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu si wakati wa kupunguza rasilimali za kufanikisha operesheni za shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO ambalo linakabiliana na janga la virusi vya Corona au COVID-19.