Mamilioni ya watoto wanaishi katika nchi ambazo takwimu kuhusu watoto hazipo au ni shida kupatikana na hivyo kuweka mustakhbali wao mashakani, imesema ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.
Kuna haja ya kuunda ushirika mpya kati ya serikali, makundi ya kulinda wanyama na mazingira pamoja na jamii katika juhudi za kushughulikia ulinzi wa mazingira kama chanzo cha kujenga uchumi endelevu.
Makwa 2017 kwa ujumla hakukuwa na mafanikio makubwa sana katika ulingo wa siasa kwa wanawake japo ushiriki wao katika masuala ya uchaguzi uliongezeka kiasi.
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu inaonyesha kama watu hao wanaishi na vitisho dhidi yao na hivyo mataifa kushindwa kutekeleza wajibu wake kuhusu suala hili.
Wabunge kutoka nchi mbalimbali duniani wanakutana makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani kubadilisha mawazo ya jinsi ya kukabiliana na suala mtambuka la uhamiaji.
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya wahanga wa mauaji ya halaiki dhidi ya wayahudi, Umoja wa Mataifa umesema silaha pekee dhidi ya vitendo kama hivyo ni elimu na uelewa kuhusu maadili ya kibinadamu.
Hatimaye mahakama ya kimataifa iliyokuwa inaendesha kesi za uhalifu uliofanyika kwenye iliyokuwa Yugoslavia, imefunga pazia rasmi leo baada ya kuhudumi kwa miaka 24.