Kadri vitisho vitokanavyo na mabadiliko ya tabianchi na biashara vinavyozidi kushika kasi, nchi nazo zinashindwa kuchukua hatua kuweka mazingira bora kwa afya ya mtoto, imesema ripoti mpya iliyochapishwa kwa ushirikiano kati mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia watoto, UNICEF na lile la afya, WHO na jarida la Lancet.