Nchini Ujerumani mafunzo mahsusi yanayotolewa na kampuni za kijerumani kwa wakimbizi yameleta siyo tu matumaini kwa wakimbizi bali pia kusaidia kujenga utangamano na jamii zinazowazunguka.
Watu zaidi ya milioni 168 kote duniani mwaka 2020 watahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi katika migogoro inayoendelea kwenye nchi Zaidi ya 50 limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu mimasuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA.
Umoja wa Mataifa umesema jamii ikiwa ni pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali, asasi za kiraia na wanaharakati wana mchango mkubwa katika vita dhidi ya UKIMWI.
Amani, usalama, upendo na mshikamano ndio msingi wa mustakabali wa dunia, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku ya Umoja wa Mataifa hii leo.
Ikiwa leo ni siku ya chakula duniani wito ukiwa ni kutokomeza njaa- na kuwa na dunia ambako chakula chenye lishe bora kinapatikana kwa bei nafuu na kwa watu wote na kila mahali, Umoja wa Mataifa unahoji iweje leo hii zaidi ya watu milioni 820 hawana chakula cha kutosheleza mahitaji yao.
Suala la ulinzi wa wakimbizi ni moja ya vipaumbele vya awali kabisa vya Umoja wa Mataifa takriban miongo saba iliyopita hata hivyo, ufurushwaji wa watu bado unazua wasiwasi mkubwa kimataifa. Taarifa kamili na Arnold Kayanda
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antinio Guterres amesema mara nyingi dunia inaiangalia amani katika mtazamo wa migogoro baina ya binadamu. Lakini amani sio tu kutokuwa na vita, ni kutengeneza mazingira ya kuwa na utangamano na utulivu kwa njia ambayo watu wataishi pamoja na kuruhusu vita kutotokea.
Hatimaye kikao cha kwanza cha mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kimeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani chini ya uongozi wa Rais wake Balozi Tijjani Muhammad-Bande kutoka Nigeria.