Katika kujibu kile kinachoelezwa kuwa tukio la ndege ya kibiashara kulazimishwa kutua katika Mji Mkuu wa Belarus, Minsk, Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Anga, ICAO, liliitisha mkutano wa dharura wa kidiplomasia siku ya Alhamisi. Je ICAO inasema nini kuhusu tukio hilo, na ina nguvu gani?