Ulaya

Vita vya kibiashara vinatishia usafirishaji wa baharini kimataifa:UNCTAD

Ripoti mpya ya kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD kuhusu usafirishaji wa njia ya baharí kwa mwaka 2018, imeonya kwamba vita vya biashara vinatishia mtazamo wa usafirishaji wa kimataifa wa bidhaa kwa njia ya baharí.

Tukiadhimisha siku ya kupinga machafuko, tufuate nyayo za Gandhi- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa dunia kufuata mtazamo na busara za Mahatma Gandhi katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga machafuko ambayo huangukia Oktoba Pili kila mwaka, siku ya kuzaliwa kiongozi huyo mashuhuri wa India aliyehamasisha vuguvugu la haki za kiraia kote duniani.

Mjadala Mkuu wa #UNGA73 wafunga pazia, Lithuania yavunja rekodi kwa hotuba fupi zaidi

Waliohutubia UNGA73:  Marais 77, wakuu 44 wa serikali, mawaziri 54, naibu mawaziri wakuu 4, Naibu Waziri 1, wawakilishi 8 wa kudumu wa  nchi kwenye Umoja wa Mataifa.

Tuimarishe ushirikiano wa kimataifa ili kunusuru uhamiaji- Grandi

Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi ametoa wito kwa mataifa kushirikiana ili kupata ufumbuzi wa suala la wakimbizi akisema makubaliano mapya  kuhusu wakimbizi  yatageuza hifadhi kuwa jibu mujarabu.

Mkataba dhidi ya tumbaku umeboresha afya ya umma- WHO

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani WHO, Dkt Tedros Adhonom Ghebreyesus ameusifu mkataba  wa kimataifa wa kudhibiti matumizi ya tumbaku, FCTC, kama moja ya mafanikio makubwa ya afya kwa jamii katika kipindi cha  miaka 20 iliyopita.

Watu bilioni 2.3 duniani hawana vyoo, hii ni hatari- WHO

Lengo la kila mkazi wa dunia kuwa na huduma za kujisafi ikiwemo choo halitafikiwa iwapo serikali hazitafanya mabadiliko ya kina na kuwekeza fedha zaidi kwenye sekta hiyo, limeonya shirika la afya ulimwenguni, WHO hii leo.