Ulaya

Bei ya vyakula duniani haikubadilika sana mwezi Agosti: FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limetoa taarifa mpya kuhusu bei ya vyakula kwa mwezi Agosti na kusema  bei kwa ujumla ilibaki palepale, haikuongezeka wala kupungua.

Acheni kupuuza haki za uzazi za wanawake na wasichana: UN

Hali ya kupuuza na kutoheshimu misingi ya kimataifa ya haki za binadamu kunatishia  haki za afya ya uzazi na kujamihiana kwa wanawake mkiwemo wenye ulemavu.

Onyo hilo limetolewa leo mjini Geneva Uswisi na wataalam wa masuala ya haki za binadamu.

Hisani si lazima , lakini thamani yake katika jamii ni kubwa:UN

Hisani, kama mawazo ya kujitolea na uhamasishaji wa kusaidia wengine, huleta uhusiano wa kweli wa kijamii na huchangia kuundwa kwa jamii imara zaidi.

Kuvuka baharí ya mediterania imekuwa kama tiketi ya kifo:UNHCR

Ikiwa ni miaka mitatu tangu picha za kutisha  za mwili wa mtoto mdogo, Alan Kurdi, akiwa katika ufukwe wa bahari nchini Uturuki  zisambae, ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia  wakimbizi, UNHCR  inaonyesha kuwa wakati huu kuvuka baharí ya Mediterania  imekua hatari zaidi inayosababisha vifo kuliko wakati mwingine wowote.