Ulaya

Safari bado ndefu usawa wa kijinsia 2030- Ripoti

Ripoti mpya kuhusu usawa kijinsia katika kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu, SDGs ifikapo mwaka 2030, imebaini kuwa bado kuna safari ndefu kufikia usawa wa kijinsia katika kipindi hicho.

Ukiadhimisha siku ya wapendao , sema marufuku ndoa za utotoni:UNFPA

Leo ni siku ya wapendao duniani , shirika la Umoja la idadi ya watu duniani UNFPA imetoa wito , tafadhali wakati unaadhimisha siku hii wakumbe wanaoingizwa katika ndoa za shuruti na kusema, imetosha, sasa ni marufuku. 

Msimu wa mafua makali wabisha hodi.

Msimu wa mafua makali tayari umebidha hodi katika nchi kadhaa huku ukinyemelea mataifa mengine, limesema shirika la afya duniani, WHO.

Radio haitokufa, na inaendelea kuwa na umuhimu mkubwa: IOM

Baadhi ya watu wamekuwa wakidai Radio ni chombo cha habari kinachokufa , lakini ukweli ni kwamba Radio imezidi kushamiri na itaendelea kuwa chombo muhimu cha mawasiliano katika jamii ndani na nje ya masuala ya kibinadamu.

Radio ngangari licha ya maendeleo ya teknolojia – Guterres

Leo ni siku ya radio duniani, ikitambua kuanzishwa kwa Radio ya Umoja wa Mataifa mwaka 1946. Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO liliridhia kuadhimishwa kwa siku hii wakati wa kikao cha bodi yake tendaji  cha tarehe 29 mwezi Septemba mwaka 2011.

Ajali ya ndege Urusi imenihuzunisha sana, poleni wafiwa:Guterres

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za ajali mbaya ya ndege iliyotokea leo karibu na mji mkuu wa Urusi Mosco ambapo abiria wote na wafanyakazi wa ndege waliokuwemo wamearifiwa kupoteza maisha.

Ukatili wa kingono watishia Wanawake na watoto wakimbizi Ugiriki:UNHCR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linatiwa hofu kubwa na taarifa kutoka kwa waomba hifadhi kuhusu hatari ya ukatili inayowakabili kwenye vituo vya mapokezi vyenye hali mbaya na kufurika  nchini Uguriki hasa kwa wanawake na watoto. 

Tochi ya Olimpiki iangazie mshikamano wa amani kimataifa:Guterres 

Juma hili maelfu ya watu na hususani wanamichezo wanakusanyika mjini PyeongChang huko Jamhuri ya Korea, kwa ni ya kushiriki mashindano ya Olimpiki ambayo ni ya kirafiki, yenye mshikamano, na ya kuheshimiana.