Licha ya kwamba idadi ya wagonjwa wa surua imepungua ikilinganishwa na miaka iliyotangulia, kasi ya kutokomeza ugonjwa huo inapungua huku milipuko mipya ikiripotiwa, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO na kituo cha Marekani cha kudhibiti na kuzuia magonjwa, CDC.