Kupunguzwa kwa muda kwa uzalishaji wa hewa ukaa kulikosababishwa na masharti ya kimataifa ya watu kusalia majumbani wakati wa janga la corona au COVID-19 hakukupunguza kasi ya kuendelea kwa mabadiliko ya tabianchi. Viwango vya gesi chafuzi vimevunja rekodi, na dunia iko njiani kuelekea hatari joto kali la kupindukia, imeonya ripoti ya mabadiliko ya tabia nchi iliyotolewa leo na mashirika mbalimbali.