Kutokana na hali mbaya zaidi ya hewa na majanga ya asili, viwango vya juu vya joto na viwango vya juu vya hewa chafuzi, ubinadamu uko kandoni mwa kuzimu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , António Guterres ameonya hii leo katika mkutano wa tabianchi uliofanyika mjini Petersberg, Ujerumani.