Mgogoro wa kimataifa wa kiafya uliosababishwa na janga la virusi vya corona au COVID-19 unaweza kuwa na athari kubwa za kiuchumi, na kusababisha upungufu wa dola bilioni 2, 000, pamoja na dola bilioni 200 kwa nchi zinazoendelea, kulingana na moja ya matarajio mabaya yaliyotolewa leo Jumatatu kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD huko Geneva Uswis.