Ulaya

Ubaguzi wa rangi bado ni jinamizi la duniani ya sasa :Guterres 

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waathirika wa utumwa na biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kutokomeza kabisa ubaguzi wa rangi unaoendelea hivi sasa. 

Tufungue bandari zetu ili shehena za dawa na vifaa viweze kusaidia kukabili COVID-19 – UNCTAD

Wakati nchi duniani zinaendelea kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19, Umoja wa Mataifa umesema sekta ya usafirishaji majini ina dhima muhimu katika hatua dhidi ya janga hilo.

IMF yatabiri mdororo wa uchumi duniani kufikia kiwango cha mwaka 2008 lakini kukwamuka mwaka 2021

Shirika la fedha duniani, IMF limesisitiza umuhimu wa hatua za pamoja duniani na mshikamano baina ya nchi zote katika vita dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 huku likisema kuwa mdororo wa uchumi kutokana na janga la sasa utafikia ule wa mwaka 2008 lakini matarajio ya kukwamuka ni mwakani.
 

Tuweke silaha chini na tupambane na adui mkubwa COVID-19:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ametoa wito wa kusitisha mapigano haraka kote duniani na nguvu zote kuzielekeza katika adui mkubwa wa sasa ambaye ni virusi vya Corona, COVID-19.

Kwenye vita watu milioni 100 wako hatarini kwa COVID-19:OCHA

Wakati virusi vya Corona , COVID-19 vikiendelea kusambaa kote duniani Umoja wa Mataifa unatiwa hofu kuhusu athari kwa watu milioni 100 wanaoishi katika maeneo ya vita na dharura nyingine ambao wanategemea misaada ya kibinadamu.

Mshikamano, matumaini na ushirikiano vyahitajika kukabili COVID-19: Guterres

Wakati hofu ikiendelea kutanda kote duniani kufuatia kusambaa kwa mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “sasa kuliko wakati mwingine wowote tunahitaji mshikamano, tumaini na utashi wa kisiasa ili kukabiliana na janga hili kwa pamoja.”

Chonde chonde wahisani tunawategemea sasa kuliko wakati mwingine wowote:UNICEF

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF ametoa rai kwa wahisani kuendelea kunyoosha mkono hasa wakati huu dunia ikikabiliana na janga kubwa la virusi vya Corona au COVID-19.

Tumeanza rasmi chanjo ya majaribio ya dhidi ya COVID-19: WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO leo limesema siku 60 baada ya sampuli za virusi vya Corona au COVID-19 kuwasilishwa kwa shirika hilo na Cina,  chanjo ya kwanza ya majaribio imeanza.

IOM/UNHCR watangaza kusitisha safari za wakimbizi sababu ya COVID-19

Wakati nchi zikibana idadi ya watu wnaoingia nchini mwao kwa sababu ya janga la kimataifa la virusi vya Corona , COVID-19 na kuweka vikwazo dhidi ya safari za kimataifa za anga , mpango wa kuwasafirisha wakimbizi kwenda kwenye makazi mapya sasa umeingia dosari.

Pamoja na kujitenga na kufunga shule tuongeze juhudi za upimaji COVID-19:WHO

Wakati virusi vya corona vikiendelea kusambaa sehemu mbalimbali duniani na kuongeza idadi ya vifo, shirika la afya ulimwenguni WHO linasema huu ni wakati wa kuongeza kasi ya upimaji.