Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHODkt. Tedros Ghebreyesus na mawanamuziki nyota duniani Lady Gaga Pamoja na Hugh Evans kutoka mradi wa raia wa kimataifa au Global Citizen Ijumaa wametangaza kwamba “ wanamuziki wengi mashuhuru duniani , wasanii wa vichekesho na wahudumu wa kibinadamu watashiriki katika tamasha maalum la kimataifa mtandaoni lijulikanalo kama “One Worl, Together at Home “ likimaanisha dunia moja, wote kwa pamoja majumbani litakalofanyika hii leo.