Ulaya

IOM na wadau wajadili usalama wa wakimbizi na wahamiaji Ubelgiji.

Mkutano wa kwanza wa nchi wanachama wa Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM), kuhusu mbinu jumuishi za uhamiaji na kuoanisha njia za wahamiaji kwenda Ulaya, umefanyika mjini Brussels, Ubelgiji na kuleta matumaini kwa mashirika yanaohusika na wakimbizi na wahamiaji.

Vaa nguo ya buluu tarehe 20 Novemba kuunga mkono kampeni ya watoto

Kuelekea siku ya watoto duniani tarehe 20 mwezi huu wa Novemba, mtoto muigizaji Millie Bobby Brown ameungana na mabalozi wema wa shirika la kuhudumia watoto duniani,  UNICEF kutumia video mahsusi kupigia chepuo kampeni ya kusongesha haki za watoto duniani. 

Wakulima na wafugaji wana ufunguo wa kuepusha usugu wa dawa- FAO

Maadhimisho ya wiki ya  kuhamasisha umma kuhusu matumizi ya viuavijasumu ikiendelea, Umoja wa Mataifa umesema wakulima wana dhima muhimu katika kupunguza usugu wa dawa hizo kwa kutumia mbinu bora za usafi katika shughuli zao za kila siku.

Njia ya kupitisha mkataba mpya wa wahamiaji sasa ni ‘nyeupe’- UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema sasa kuna matumaini makubwa ya kupitishwa kwa mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbiz na wahamiaji, GCM mwezi ujao.

Uholanzi ondoeni ubaguzi wa rangi katika mfumo wa ustawi wa jamii: UN

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameelezea wasiwasi mkubwa juu ya ubaguzi wa rangi katika mfumo wa ustawi nchini Uholanzi, wakitumia mfano wa tukio la familia moja ya wakimbizi wenye asili ya Afrika wanaoishi nchini  humo ambayo ilinyang’anywa usimamizi wa watoto wao.

Sekta ya ubunifu wa nguo nayo yahaha kulinda mazingira

Wakati dunia ikihaha kusaka mbinu za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira, sekta ya ubunifu wa mitindo nayo imeshachukua hatua ili kuhakikisha bidhaa zake haziharibu mazingira.

Mataifa yakishikamana, matumaini na suluhusu vinawezekana:Guterres

Kuanzia migogoro, na matatizo ya kiuchumi, hadi maradhi na mabadiliko ya tabia nchi, changamoto hizi za dunia zinahitaji sasa kuliko wakati mwingine wowote mshikamano imara wa kimataifa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwaasa viongozi wa dunia kwenye kongamano la kimataifa la Amani lililofanyika leo Jumapili mjini Paris Ufaransa kuadhimisha miaka 100 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia.

Uwekezaji vijijini ni muarobaini wa amani ya kudumu duniani- IFAD

Kuelekea jukwaa la amani litakaloanza kesho huko Paris, Ufaransa, Rais wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD Gilbert F. Houngbo, amesema atatumia kusanyiko  hilo kuwaeleza viongozi wa dunia juu ya umuhimu wa kuwekeza vijijini.

Kama ng’ombe wangekuwa nchi, nchi hiyo ingekuwa ya tatu kwa uchafuzi wa mazingira duniani.

Pengine si wengi wanaoiingia katika mghahawa unaouza mathalani burger yaani nyama iliyofunikwa kwa mkate, wanaowaza kuwa chakula hicho wanachokinunua ni sawa na kushiriki katika kuharibu mazingira. Harakati za binadamu katika kutengeneza nyama ni njia mojawapo za uharibifu unaoacha alama duniani.

Gharama ya juu ya nyumba EU yakatisha tamaa vijana- Ripoti

Hatma ya mamilioni ya vijana kupata ajira kwenye miji mikuu ya Muungano wa Ulaya, EU iko mashakani kutokana na bei za nyumba kuwa ni za juu kupita kiasi sambamba na kodi ya pango.