Asia Pasifiki

Siku ya afya duniani 2009 kuadhimishwa 07 Aprili

Ijumanne ya tarehe 7 Aprili huhishimiwa kimataifa kuwa ni Siku ya Afya Bora Duniani. Taadhima za 2009 zitalenga zaidi kwenye zile juhudi za kuimarisha usalama wa vifaa na nyenzo za kuhudumia afya ulimwenguni, na pia kwenye uwezo wa wahudumia afya katika mazingira ya tiba ya dharura.

KM asikitishwa na urushaji wa kombora angani na Korea Kaskazini

Ofisi ya Msemaji wa KM, kwenye ripoti iliotoa Ijumapili kwa waandishi habari, kuhusu kitendo cha kurusha kombora angani kilichofanywa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (Korea Kaskazini) hapo jana, taarifa hiyo ilibainisha masikitiko aliyokuwa nayo KM Ban Ki-moon juu ya kitendo cha Korea Kaskazini, ambacho alisema ilikwenda kinyume kabisa na nasaha za jumuiya ya kimataifa.

Mawaziri wa Afya wakubaliana Beijing kuharakisha udhibiti bora wa TB sugu

Mkutano wa siku tatu, ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), kwa ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Umma wa Uchina pamoja na Taasisi za Bill na Melinda Gates, ulifanyika Beijing wiki hii, kwa makusudio ya kushauriana juu ya mradi mpya wa utendaji, utakaofaa kutekelezwa kipamoja ili kudhibiti bora maradhi ya kifua kikuu, hususan kwenye yale mataifa yanayosumbuliwa zaidi na ugonjwa huo.

Mataifa wanachama kuashiria mafanikio ya kuridhisha kuhusu Mkutano wa Durban

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu imearifu kuwa wawakilishi wa serikali wanachama wana imani ya kupatikana mafanikio ya kuridhisha katika kikao kijacho cha mapitio kuhusu masuala ya ukabila, ubaguzi wa rangi, matatizo ya chuki dhidi ya wageni na utovu wa kustahamiliana kitamaduni.

Jaji wa Afrika Kusini ameteuliwa kuongoza tume ya uchunguzi juu ya ukiukaji sheria za kiutu Ghaza

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu limetangaza kumteua Jaji Richard Goldstone wa Afrika Kusini kuongoza ile tume huru ya kuchunguza ukweli kuhusu ukiukaji wa sheria ya kimataifa juu ya haki za binadamu, na uvunjaji wa haki za kiutu, uliofanyika wakati mgogoro wa eneo liliokaliwa la WaFalastina la Tarafa ya Ghaza ulipopamba mnamo miezi kichache iliopita.

Mabomu yaliotegwa yaendelea kuhatarisha watoto, kuonya UNICEF

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kwamba mabomu yaliotegwa ardhini, pamoja na mabaki ya silaha zilizowachwa kwenye eneo la mapambano baada ya vita kumalizika, ni viripuzi vinavyoendelea babdo kuhatarisha maisha ya watoto katika kadha wa kadha ulimwenguni.

Wabuni sera za kimataifa wahimizwa na FAO kuwashirikisha wakulima kwenye mijadala ya Mkataba wa Kyoto

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limetoa taarifa yenye kuwahimiza wabuni sera za kimataifa kuhusu udhibiti wa athari za mabadiliko ya hali hewa duniani kujumuisha suala la kilimo pale wanapozingatia mkataba mpya utakaofuatia Mkataba wa 1997 wa Kyoto, baada ya kukamilisha muda wake.

Siku ya Kukumbushana Ugonjwa wa Autism yaadhimishwa na UM

UM leo unaadhimisha Siku ya Kukumbushana juu ya Ugonjwa wa Akili wa Watoto au kwa Kiingereza chake ugonjwa wa autism.

Idadi ya majongoo ya pwani imepungua ulimwenguni, yahadharisha FAO

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limehadharisha kwenye ripoti ya kuwa akiba ya majongoo wa pwani, au madondo, inaelekea kupungua ulimwenguni kwa kima cha kushtusha, hasa katika maeneo ya Afrika na kwenye Bahari ya Hindi ambapo uvuvi wa majongoo hawa imekiuka ada.

Wajumbe wa nchi 30 ziada wakutana Beijing kuzingatia tiba ya TB sugu

Mawaziri wa afya pamoja na wajumbe wa kutoka nchi 30 ziada wameanza kikao cha siku tatu mjini Beijing, Uchina kuzingatia namna ya kukabiliana na tatizo la kuemewa na maradhi sugu ya kifua kikuu yasiokubali dawa.